Adhabu ya Juma Nyosso kwa kosa la udhalilishaji.

Nahodha wa timu ya Mbeya City, Juma Nyosso

Jioni ya September 27 ilikuwa ni siku ambayo wadau wengi wa soka walikuwa wakijadili kuhusiana na tukio la kidhalilishaji, lilitokea katika mechi ya Azam FC dhidi ya Mbeya City, mechi ambayo ilipigwa katika uwanja wa nyumbani wa Azam FC Azam Complex Mbande Chamazi.
Tukio lililotokea katika mechi hiyo ambalo kila mpenda soka Tanzania hakulipenda ni beki wa kati na nahodha wa klabu ya Mbeya City Juma Nyoso kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji nahodha wa Azam FC John Bocco, baada ya tukio kufanyika kila mtu aliongea lake ila Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi alithibitisha kupitia account yake rasmi ya twitter kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya Juma Nyoso.

Taarifa mpya kutoka katika kamati ya uendeshaji wa Ligi, zinaeleza kukaa chini na kupitia kosa la Juma Nyoso na kuamua kumpa adhabu ya kumfungia kucheza soka katika kipindi cha miaka miwili pamoja na faini ya milioni 2. Kamati hiyo imefikia maamuzi hayo kutokana na Juma Nyoso kuwa mkosefu sugu wa kitendo hicho cha kidhalilishaji katika mchezo wa soka.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment