Kondomu yenye umbo la chupi Uganda





Kuna aina mpya kondomu ya wanawake ambayo inapigiwa upatu na shirika moja nchini Uganda.
Kondomu hii inaumbo la suruali ya ndani ya wanawake.

Inaweza kuvaliwa siku nzima na wanawake sawa na chupi aina ya ''g-string''
Kondomu hiyo ya kisasa maarufu kama ''panty condom'' itasaidia wanawake haswa wanaposhiriki tendo la ndoa pasi na kutarajia ima ni ghafla ama ubakaji.

Haswa shirika linayoinadi kondomu hii ya kipekee inasema kuwa inanuiwa kuzuia usambazaji wa magonjwa mbalimbali kwa ngono ikiwemo UKIMWI.

Hata hivyo mamlaka ya madawa nchini Uganda inasema kondomu hiyo bado haijapimwa kuona kama inafikia viwango vya kitaifa.

Source: BBC Swahili
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment