Kisa cha abiria 900 kukwama kwenye Treni hiki hapa.



Dar es Salaam.Watu zaidi ya 900 wamekwama katika stesheni ya Pugu jijini Dar es Salaam tangu jana usiku baada ya treni ya mizigo kuangusha mabehewa na kuzuia njia.

Abiria hao waliokuwa wanaelekea katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Mwanza na Kigoma wameshindwa kuondoka na treni yao kupitia reli ya kati hawajui hatima yao hadi Mwananchi ilipowasili katika eneo la tukio kwa kuwa hawajawaona viongozi wa Shirika la Reli (TRL).
Taarifa zinasema ajali ya treni ilitokea jana usiku eneo la Mpiji hivyo isingewezekana kuendelea na safari hivyo ikabidi wasimame stesheni ya Pugu wakitaraji hadi leo asubuhi kadhia hiyo ingekuwa imemalizika.

Mwananchi Digital imeshuhudia abiria hao wakiwa katika hali dhohofu hasa kwa wazee na watoto kutokana na njaa.

Sintofahamu imeongezeka miongoni mwa abiria hao kwani hadi Mwananchi Digital inaondoka eneo hilo, hakuna taarifa ya kinachoendelea kutoka kwa mamlaka husika hivyo haijulikani muda ama lini wataondoka katika eneo hilo.
Share on Google Plus

About Aldo Simon

0 comments:

Post a Comment